||

WOCHATA

WOCHATA

WOCHATA

WOCHATA

WOCHATA

WOCHATA

Friday, 10 October 2014

TRA: USAJILI MPYA WA PIKIPIKI


Serikali imeamua kuanzisha usajili mpya wa namba za pikipiki (aina zote za pikipiki zenye magurudumu mawili na zaidi) ili kurahisisha usimamizi na utawala wa vyombo vya moto. Utaratibu mpya wa Usajili unaanza rasmi tarehe 1/10/2014. Mmiliki anapewa muda wa miezi sita kubadilisha usajili bila adhabu.

Usajili huu utahusu vyombo vya moto aina ya pikipiki vyenye magurudumu mawili au zaidi. Pikipiki  kwa ajili ya biashara zinatakiwa kubandikwa vibao vya namba ya rangi nyeupe na kwa ajili shughuli binafsi zitabandikwa vibao vya namba za rangi ya njano.

Usajili huu utafanyika katika ofisi zote za TRA   na mmiliki anatakiwa kwenda TRA na kadi halisi ya pikipiki na Tshs.10, 000/- kwa ajili ya kadi mpya.

Wito unatolewa kwa wamiliki wote wa pikipiki ikiwa ni pamoja na zile za magurudumu matatu au manne maarufu kwa jina la Bajaji, wafike katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kukamilisha usajili wa vyombo wanavyomiliki.

Tuesday, 30 September 2014

PSI NA TPSF KUWAWEZESHA WANAWAKE TANGA

Zikiwa zimebaki siku 14 tu kufanyika kwa ile Shughuli ya Wochata Jol inayosubiriwa kwa hamu na wakazi wa mkoa wa Tanga. PSI na TPSF wameahidi kuja kuwaelimisha Wanawake wa Tanga na kuwawezesha kupata fursa za kupata elimu ya Afya ya uzazi (PSI) na Ujasiriamali (TPSF).
PSI ni moja ya mashirika makubwa duniani yanayotoa huduma za afya hapa nchini. Ambapo TPSF wao ni taasisi ya sekta binafsi Tanzania.

Mashirika haya mawili yatatoa Wawakilishi kuja kuwaelemisha Wanawake wa Tanga katika Shughuli ya Wochata Jol itakayofanyika tarehe 14 Oktoba 2014, katika ukumbi wa Regal Naivera Tanga.



MIRIAM MIGOMBA: " PATAKUWA HAPATOSHI TAREHE 14 OKTOBA 2014"

Mwanadada Mc mahiri, Miriam Migomba amezungumzia tukio la wochata jol kuwa litaweka historia na kubadilisha maisha ya wanawake wa Tanga. Akiongea kwa njia ya simu na blogu hii amesema amejiandaa vya kutosha kuja kutoa somo kwa watakaoshiriki siku hiyo.

Mwanadada Miriam Migomba 

"Nachoweza kusema wanawake wenzangu wa Tanga, watambue kuwa kama hatuna desturi ya kukumbushana na kupeana mikakati ya kujiondolea umaskini sisi wenyewe, basi kamwe hakuna mtu wa kuja kutuondolea" alisema.
Amesisitiza Wanawake kuungana na kuweza kufanya harakati za kujikomboa na umaskini pamoja. Hili ni tukio la pili kuandaliwa na kikundi cha umoja wa wanawake Tanga (Wochata) baada ya awali kuandaa event kama hiyo tarehe 3 mei  mwaka huu. Katika shughuli hiyo Wochata waliwaalika watoa mada Regina Mwaleka (mada ya ndoa) na Joy Nyambogo (mada ya Ujasiriamali). Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Madam Latifa Shehoza.


Mgeni rasmi, Madam Latifa Shehoza (katikati) akiwa na Mtangazaji maarufu Regina Mwaleka (Kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Wochata Risala A. Samiji katika Shughuli ya Wochata iliyofanyika mwezi mei 3, 2014.